1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUganda

Uganda yamkamata mkuu wa wanamgambo anayedaiwa kuua watalii

3 Novemba 2023

Mamlaka nchini Uganda imefahamisha imemkamata mkuu wa kikosi cha wanamgambo wanaoshukiwa kwa mauaji ya watalii wawili na mwongozi wao katika mbuga ya wanyama mwezi uliopita.

https://p.dw.com/p/4YM3y
Mkuu wa wanamgambo wa ADF aliyekamatwa na maafisa wa polisi Uganda anadaiwa kuhusika na mauaji ya watalii wawili hivi karibuni nchini Uganda.
Mkuu wa wanamgambo wa ADF aliyekamatwa na maafisa wa polisi Uganda anadaiwa kuhusika na mauaji ya watalii wawili hivi karibuni nchini Uganda.Picha: Alain Uaykani/Xinhua/IMAGO

 Msemaji wa Jeshi la Uganda Deo Akiiki amesema mtu huyo aliyefahamika kwa jina moja la Njovu, ndiye manusura pekee wa operesheni ya kijeshi ya siku ya Jumanne dhidi ya kikosi cha wanamgambo wa Allied Democratic Forces (ADF) ambapo wapiganaji wengine sita waliuawa.

Akiiki amesema Njovu alikutwa na baadhi ya mali za watalii waliouawa ambao walikuwa raia wa Uingereza na Afrika Kusini, pamoja na kitambulisho cha mwongozi wao raia wa Uganda, na kwamba mshukiwa huyo anatarajiwa kufikishwa Mahakamani.