Uganda kuzindua awamu ya tatu ya utafiti wa mafuta
3 Januari 2025Uganda inatarajiwa kuzindua awamu ya tatu ya utoaji leseni ya utafiti wa mafuta katika mwaka wa fedha unaoanza mwezi Julai. Hayo yamesemwa na waziri wa nishati na madini Ruth Nankabirwa katika taarifa aliyoitoa jana Alhamisi.
Uganda iligundua mafuta ghafi katika bonde la Albertine Graben karibu na mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo karibu miongo miwili iliyopita, lakini shughuli za uchimbaji zilicheleweshwa.
Soma: Museveni aapa kuendeleza mradi wa mafuta licha ya upinzani wa Bunge la Ulaya
Mnamo mwezi Agosti, nchi hiyo ilisema wanajiolojia wa serikali walikuwa wakifanya tafiti za awali za mafuta katika mabonde mawili mapya upande wa kaskazini na kaskazini mashariki.
Wakati huo huo waziri Nankabirwa ametangaza kuwa wizara imempata mshindi wa zabuni ya kuendeleza mgodi mkubwa wa shaba magharibi mwa nchi hiyo.