SiasaUfilipino
Ufilipino na China zafikia makubaliano kuzima mgogoro
21 Julai 2024Matangazo
Katika taarifa yake Wizara ya mambo ya nje ya Ufilipino imesema makubaliano hayo yalifikiwa baada ya mfululizo wa mashauriano mjini Manila, kufuatia kuongezeka kwa mvutano katika eneo hilo.
Soma pia: Ufilipino yaishutumu China kutaka kupoka eneo la bahari
Taarifa hiyo imedokeza kwamba pande zote mbili zinaendelea kutambua hitaji la kuepuka mgogoro katika Bahari ya Kusini ya China na kukabiliana na tofauti zao kupitia mazungumzo na majadiliano na kwamba makubaliano hayo hayataibua chuki na kuathiri misimamo ya wengine katika eneo linalozozaniwa.
China, ambayo inadai karibu Bahari nzima ya China Kusini ni mali yake, imechukua hatua za kibabe katika eneo hilo katika miaka ya hivi karibuni ikizuia mataifa mengine kulifikia au kulitumia.