Ufaransa yashutumiwa kusaidia ukandamizaji wa al-Sissi
2 Julai 2018Matangazo
Uchunguzi huo ulioidhinishwa na makundi manne ya haki za binadamu ya Ufaransa na Misri, uligundua kwamba mauzo ya silaha yameongezeka kutoka euro milioni 39.6 hadi bilioni 1.3 kati ya mwaka 2010 hadi 2016.
Wamedai kuwa makampuni ya Ufaransa ni washirika katika kile walichokiita, ukandamizaji usiokoma, tangu Sissi alipomuondoa madarakani rais mwenye anayefuata misimamo ya dini ya Kiislamu, Mohammed Mursi mwaka 2013.
Ripoti hiyo imedokeza kuhusu makampuni yanayouza teknolojia inayotumika katika kuingilia kati data za mawasiliano ya umma na udhibiti wa makundi ya watu zinazotumiwa katika mfumo wa uchunguzi ambao mamia kwa maelfu ya wapinzani na wanaharakati wamekamatwa.