Ufaransa yafunga viwanja 12 vya ndege, Ikulu ikihofia ugaidi
20 Oktoba 2023Matangazo
Hii ni mara ya tano katika kipindi cha siku chache zilizopita.
Waziri wa sheria wa Ufaransa, Éric Dupond-Moretti, amesema kuwa miongoni mwa wanaotoa taarifa hizo ni vijana wadogo wasiowajibika na kuongeza kuwa ni wazazi watakaolazimika kulipia hasara kubwa ya kifedha inayotokana na vitendo hivyo.
Soma zaidi: Polisi wafanya msako baada ya kitisho cha bomu Ufaransa
Waziri Moretii amesema hilo halikubaliki na kwamba ni kuzusha hali ya hofu isiyohitajika nchini humo.
Vitisho vya mabomu vimeongezeka nchini Ufaransa ambayo imetangaza hivi karibuni kuwa katika kiwango cha juu zaidi cha tahadhari kwa matendo ya kigaidi.