SiasaNiger
Ufaransa inapanga kuwaondoa raia wake nchini Niger
1 Agosti 2023Matangazo
Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa maandalizi ya shughuli hiyo ya kuwaondoa kati ya raia 500 hadi 600 wa Ufaransa walioko nchini humo yanaendelea. Kulifanyika maandamano ya kuunga mkono mapinduzi hayo mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo waandamanaji walikusanyika mbele ya ubalozi wa Ufaransa huku baadhi wakiripotiwa kuweka bendera za Niger na Urusi katika ubalozi huo.
Italia yatangaza kutuma ndege maalumu Niger kuwaondoa raia wake
Ufaransa ina karibu wanajeshi 2,500 nchini Niger. Vile vile, nchi hiyo ni muhimu kwake kwa sababu ya utajiri wake wa madini ya urani. Italia pia imetangaza kwamba itatuma ndege maalum nchini humo kwa ajili ya kuwaondoa raia wake.