Uchunguzi kuhusu mauaji ya halaiki Rwanda kuanzishwa tena
21 Juni 2023Matangazo
Vyanzo kadhaa vimeliambia shirika la habari la AFP kwamba uamuzi huo umekuja baada ya wachunguzi mwaka jana kuifunga kesi hiyo.
Mashirika kadhaa na watu walionusurika mauaji ya Kimbari nchini Rwanda yaliyofanywa dhidi ya jamii ya Watutsi, katika milima ya Bisesero, magharibi mwa Rwanda, kwa muda mrefu wamekuwa wakiutuhumu ujumbe maalum wa jeshi la Ufaransa na serikali kuwa washirika wa mauaji hayo,wakisema wanajeshi hao walifanya makusudi kushindwa kuwalinda wahanga kwa siku tatu wakati mauaji yakiendelea.
Mamia ya Watutsi waliuwawa katika eneo hilo la milima ya Bisesero kati ya Juni 27 na 30 mwaka 1994.