Uchaguzi Mkuu wa Tanzania kufanyika Oktoba, 28
21 Julai 2020Ibara ya 41 kifungu cha nne cha katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania 1977 pamoja na marekebisho yake, ikiambatana na vifungu kadhaa katika sheria ya uchaguzi pamoja na sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa sura ya 292, inatoa kibali kwa tume hiyo kutangaza ratiba ya uchaguzi.
Akitumia takriban dakika mbili kuutangazia umma ratiba ya uchaguzi mwenyekiti wa NEC jaji mstaafu wa mahakama ya rufaa Semistokles Kaijage amesema, mbali na mambo mengine kampeni za uchaguzi zitaanza rasmi Agast 26 hadi Oktoba 27 mwaka huu, huku tarehe ya uchaguzi ikianguakia siku ya jumatano ambayo ni Oktoba 28.
Tume ya uchaguzi yatoa maelezo bila ya kuruhusu maswali
Aidha tume hiyo haikutaka kuruhusu maswali kupeleka uchaguzi kuwa siku ambayo itakuwa ni katikati ya juma, licha ya wanahabari kujiandaa na maswali ya kuhoji zaidi. Itakumbukwa kuwa chaguzi zilizopita tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi takriban miongo miwili sasa, tanzania ilizoeeleka uchaguzi kufanyika jumapili ya mwisho wa mwezi wa kumi, hatua ilioleta mazoea miongoni mwa wananchi kuwa huenda hata uchaguzi wa mwaka huu ungelifanyika katika tarehe hizo.
Rais John Magufuli wa taifa hilo atawania muhula wa pili , baada ya kuteuliwa kuwa mgombea wa chama tawala mapema mwezi huu. Magufuli ambaye alichaguliwa kuwa rais mwaka 2015, katika muhula wake wa kwanza alishutumiwa kubana uhuru wa kujieleza, akizidisha uongozi wa mkono wa chuma na kuzuwia taarifa za janga la virusi vya corona nchini humo.
Soma zaidi: Membe kuwania urais wa Tanzania kupitia ACT-Wazalendo.
Nchi hiyo haijatoa taarifa rasmi za kesi za maambukizi ya virusi vya corona tangu Aprili 29, tofauti na nchi jirani haijachukua hatua zozote kupambana na virusi. Jana, Magufuli alisisitiza madai yake kuwa Tanzania haina tena wagonjwa wa COVID - 19, na kuwataka watalii wa kimataifa kutembelea nchi hiyo.