Washington DC yasalia tulivu kabla ya kivumbi
5 Novemba 2024Mji wa Washington DC haujashuhudia hekaheka zake za kawaida tangu asubuhi ya leo, siku ambayo Wamarekani wanateremka vituoni kumchagua rais mpya. Kulikuwa na magari machache tu barabarani, huku idadi ndogo ya watu wakionekena wakifanya shughuli zao.
Soma pia: Harris ama Trump! Wamarekani wamchagua rais wao
Akizungumza na DW, dereva mmoja mkongwe wa texi amesema, tangu Jumatatu, mji umesalia kimya. Na hakuonekana mwenye furaha na inaeleweka wazi ni kwa nini. Alilalamika kuwa kila mmoja anafuatilia uchaguzi kutokea majumbani. Ina maana madereva wa texi hawana kazi nyingi ya kufanya.
Baadhi ya majeshi kwenye Mtaa wa Pennylvania, Barabara ambayo inapatikana Ikulu ya White House, zilianza maandalizi ya usalama tangu Ijumaa, huku wafanyakazi wakiweka vizuizi kwenye sehemu za mbele kwa kutumia mbao nyepesi. Majengo ya ofisi Pamoja na migahawa pia inachukua hatua za tahadhari.
Soma pia: Harris, Trump wafanya kampeini za mwisho Pennsylvania
Mwanamke mmoja aliyekuwa anapita karibu na ua unaoizingira Ikulu ya White House anasema bila shaka huwa pana hofu inayoshuhudiwa karibu na DC kwamba kitu kama vurugu za Capitol huenda kikatokea tena. Lakini anaiambia DW kuwa kwa jumla anafikiri watu watakuwa sawa.
Washington yataka kuzuia marudio ya Januari 6
Washington imekuwa katika tahadhari kubwa kabla ya uchaguzi wa leo kwa sababu kumbukumbu ya mchakato uliopita wa ubadilishanaji Madaraka bado ipo katika akili za watu. Mnamo Januari 6, 2021, wakati Bunge la Marekani liliidhinisha ushindi wa Joe Biden, umati wenye ghadhabu wa wafuasi wa Donald Trump na watu wenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia ulivamia jengo la Bunge la Capitol Hill. Nusu mwaka kabla ya hapo, wakati wa maandamano ya vuguvugu la Black Lives Matter ya Mei na Juni 2020, maduka kadhaa na biashara zilizoko kandoni mwa Barabara mjini Washington ziliharibiwa.
Maafisa wa jiji hilo Pamoja na mashirika ya jimbo na ya kiserikali yameapa mara hii kutojikuta katika hali kama iliyotokea huko nyuma na kumlinda kila mmoja katika wiki hii ya uchaguzi na baada ya mchakato huo. Mkuu wa Polisi Pamela A. Smith amesema karibu polisi 3,300 wa Washington DC watafanya kazi kwa zamu ya saa 12- kuhakikisha kuwa kuna maofisa wa kutosha mitaani na katika kila kona ya Wilaya hiyo.
Soma pia: Ufuatiliaji wa Afrika katika uchaguzi wa Marekani
Mgombea wa urais wa chama cha Democratic na makamu wa rais wa sasa Kamala Harris yuko leo mjini Washington. Naye Donald Trump, mgombea wa Republican atakuwa West Palm Beach, Florida, sio mbali na makazi yake ya Mar-a-Lago.
Ripoti hii ilitafsiriwa kutoka kwa Kiingereza