UAE yaitolea mwito Syria kujizuwia na vurugu
8 Desemba 2024Matangazo
Akizungumza katika mkutano wa Manama, Gargash ambae ni mshauri wa kidiplomasia wa rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu amesema anatumai raia hao watafanya kazi pamoja kuzuwia dunia kushuhudia tena mzozo nchini humo.
Waasi wa Syria waingia Damascus, wasema Assad amekimbia
Rais Assad hadi sasa hajulikani aliko na Gargash alikataa kuthibitisha au kukanusha iwapo rais huyo ataomba hifadhi UAE. Huku hayo yakiarifiwa muungano wa waasi nchini Syria umesema unafanya kazi kukabidhi madaraka kwa baraza la mpito.