Tuzo ya Nobel ya Uchumi yaenda kwa Wamarekani
8 Oktoba 2018Matangazo
Jopo la tuzo hiyo limesema wanauchumi hao, William Nordhaus ambaye ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Yale na Paul Romer, aliyekuwa mkuu wa masuala ya uchumi katika Benki ya Dunia na sasa ni mhadhiri katika Chuo cha Biashara mjini New York, wameweza kuyapatia jibu maswali magumu ya wakati huu, juu ya namna ya kutengeneza uchumi endelevu na wa muda mrefu.
Jopo hilo limeongeza kuwa watu hao wawili wamepanua upeo wa uchambuzi wa kiuchumi, wakifafanua vyema namna uchumi wa masoko unavyoingiliana na mazingira asilia na ujuzi wa watu.
Wote wawili, Nordhaus na Romer, wamekuwa wakitajwa kwa muda mrefu kama wastahiki wa tuzo hiyo. Tuzo hiyo inaambatana na kitita cha Dola milioni moja.