Tuzo ya Nobel: Mabalozi wa Amani Afrika
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ndiye mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel – mshindi wa kumi barani Afrika. Ametunukiwa kwa juhudi zake za upatanisho. Tuzo ya kwanza ya Amani ya Nobel ilienda Afrika mnamo 1960.
Kavalia kofia ya chui kupokea tuzo
Albert Luthuli alikuwa Mwafrika wa kwanza kupokea Tuzo ya Amani ya Nobel mnamo 1960 kwa sera yake ya amani dhidi ya ubaguzi wa rangi huko Afrika Kusini. Wakati Rais wa ANC akiheshimiwa, harakati za ukombozi zilizuiliwa na serikali ya kibaguzi, kumpiga marufuku Luthuli.Hakuweza kupokea tuzo hiyo hadi mwaka mmoja baadaye- marufuku ya kusafiri ikaondolewa kwa siku kumi, Luthuli alisafiri kwenda Oslo.
Miongoni mwao makasisi
Askofu Mkuu Desmond Tutu alikuwa kiongozi wa maadili wa Afrika Kusini na alifanya kampeni ya kutetea haki za binadamu na alipinga ubaguzi. Kwa kauli ya Tutu "Sisi ni taifa la upinde wa mvua". Mnamo 1984, padri wa Kianglikana alipokea tuzo hiyo Olso. Kwa ucheshi wake hakuwa tu rafiki wa karibu wa Mandela, lakini aliithaminiwa ulimwenguni kote, pia Dalai Lama.
Amandla hatimaye yupo huru
Picha hii ilienea ulimwenguni kote: Wakati shujaa wa kupinga ubaguzi wa rangi Nelson Mandela alipoachiliwa huru mnamo 1990 baada ya kuishi miaka 27 gerezani, Afrika Kusini ilisherehekea ilikuwa kihistoria. Hatua yake ya kupinga ukandamizaji bila kuchoka ilisababisha demokrasia Afrika Kusini mnamo 1994. Mwaka mmoja kabla, Mandela, pamoja na Waziri Mkuu Fredrik Willem de Klerk, walishinda tuzo hiyo.
Wapinzani wawili waungana kwa amani
Ujasiri, uvumilivu na maazimio ulisababisha lengo la wapinzani hawa: Nelson Mandela na Waziri Mkuu wa Afrika Kusini Fredrik Willem de Klerk walipewa Tuzo ya Amani ya Nobel mnamo 1993 - hata kabla ya uchaguzi ambao Mandela alichaguliwa kuwa rais wa kwanza mweusi. Mapinduzi ya amani yalifanikiwa, lakini mchakato wa amani una shaka shaka licha ya kuwepo kwa demokrasia.
Kwa minajili ya amani ulimwenguni
Kofi Annan alifahamika kama balozi wa amani. Mwanadiplomasia wa Ghana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, pamoja na umoja huo, alitunukiwa Tuzo ya Nobel mnamo 2001 kwa kujitolea kwake kudumisha amani ulimwengu. Licha ya jitihada zake alikabiliwa na doa: Kutokana na madai kwamba Umoja wa Mataifa ulifumbia macho mauaji ya kimbari nchini Rwanda, Annan alikiri kushindwa baadaye.
Mama wa miti
Mnamo 2004, mwanamke mweusi alipewa Tuzo ya Amani ya Nobel kwa mara ya kwanza: Wangari Maathai. Profesa kutoka Kenya alipigania haki za wanawake dhidi ya umaskini katika nchi yake. Akiwa naibu waziri wa Mazingira alipewa jina la utani "Mama wa Miti". Alisherehekea tuzo hiyo kwa njia yake mwenyewe, aliandika kwenye kitabu chake "Nilipanda mti."
Tuzo ya wanawake
Mwaka wa 2011, wanawake watatu walitunukiwa kwa pamoja. Rais wa Liberia Ellen Johnson-Sirleaf (kulia) na mshirika wake, mwanaharakati wa haki za binadamu Leymah Gbowee (katikati) na mwandishi wa habari Tawakkul Karman kutoka Yemen. Wanawake hao wawili kutoka nchi ya Afrika Magharibi, Liberia walitunukiwa kwa juhudi zao za kuokoa nchi yao kutokana na ghasia za wenyewe kwa wenyewe.
Wanamuita "Daktari wa Miujiza"
Daktari wa Kongo na mtetezi wa haki za binadamu Denis Mukwege ameifanya iwe kazi ya maisha yake kuwasaidia waathirika wa unyanyasaji wa kingono. Kwa miaka mingi, daktari huyu wa wanawake amekuwa daktari bingwa wa upasuaji wa Hospitali ya Panzi eneo la Bukavu, ambayo aliianzisha 1999. Yeye huwapa matumaini na ujasiri waathiriwa. Alikabidhiwa Tuzo ya Nobel mwaka 2018, pamoja na Jesidin Nadia Murad.
Mwanzo wa mapinduzi kwa vijana
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ana sababu ya kusherehekea: Atatunukiwa mwaka huu kwa kujitolea kuleta amani Ethopia na Eritrea. Mbinu yake ya kuleta maridhiano Ethopia inavutia, licha ya safari ndefu na changamoto mbalimbali. Ujasiri wa kuleta mageuzi katika taifa lenye makabila mengi imetoa taswira njema. Abiy atapokea Tuzo ya Nobel huko Oslo, Desemba 10.