Tuzo ya Haki ya Maisha yaenda kwa Daktari wa DRC
26 Septemba 2013Matangazo
Daktari Mukwege ametambuliwa kutokana na kazi yake ya kuwatibu wanawake waliyoathiriwa na vurugu za kingono wakati wa vita, na pia ujasiri wake wa kuzungumzia vyanzo vya vurugu hizo. Dk.Mukwege anaendesha hospitali mjini Bukavu na amekwisha wahudumia wanawake karibu elfu 40 waliobakwa nchini Kongo. Iddi Ssessanga amezungumza na bibi Tereza Mima kutoka Tume ya haki na amani mjini Bukavu kuhusiana na tuzo hii kwa Dk. Mukwege, anaelezea umuhimu wake kwa watu wa Kongo. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga
Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman