Tuzo ya DW ya Uhuru wa Kujieleza ya 2017
3 Mei 2017Waandishi wa habari hao ni wanachama wa chama cha waandishi wa habari wa Ikulu. Mkurugenzi mkuu wa Deutsche Welle, Peter Limbourg, atampa rais wa chama cha waandhishi cha ikulu WHCA, tunzo katika mkutano wa kimataifa wa vyombo vya habari utaofanyika hapa Ujerumani mjini Bonn mwezi wa Juni.
Waandishi wa habari wanaoripoti kutoka Ikulu ya White House wamekuwa wakikabiliwa na matatizo mbalimbali tangu rais wa Marekani Donald Trump kuingia madarakani. Rais huyu amekuwa akisema kuwa waandishi wengi wanaripoti habari za uongo, hasa zile zinazomhusu yeye. Chama cha waandishi wa habari wanaoripoti kutoka Ikulu wa chama cha WHCA wameanzisha njia za kuripoti habari za sera ya uongozi mpya wa Marekani.
Mkurugenzi mkuu wa Deutsche Welle, Peter Limbourg, alisema kuwa wanaamini muundo wa demokrasia wa Marekani. Aliongezea kusema pia waandishi wa habari wanaoripoti kutoka Ikulu ndio wanaodhibiti wale waliokuwa na mamlaka.
Rais wa chama hicho Jeff Mason alisema kuwa chama cha waandishi wa habari wa Ikulu wanashukuru kwa heshima kubwa waliyopewa kwa kutunukiwa na shirika la habari la Deutsche Welle tunzo ya uhuru wa kujieleza ya mwaka huu.
"Chama cha WHCA kinapigana kila siku kwa ajili ya haki za waandishi wa habari wanaoripoti habari kuhusu viongozi wenye sera zinazoathiri dunia nzima. Hatupewi uhuru wa vyombo vya habari Marekani, japo kuwa uhuru wa kujieleza ni sehemu moja ya katiba ya Marekani. Lazima tupigane ili uhuru huo uwepo bila ya kujali nani yupo madarakani," alisema Jeff Mason.
Shirika la habari za kimataifa la Ujerumani Deutsche Welle lilianzisha tunzo ya Uhuru wa kujieleza miaka miwili iliyopita kwa kuheshimu wale wanaokuwa na uhuru wa kujieleza na haki za binadamu katika mbinu bunifu.
Mwandishi wa blogu wa Saudia Raif Badawi aliyekuwa kifungoni alipokea tunzo hiyo mwaka 2015. Mke wake Ensaf Haidar alipokea tunzo hiyo kwa niaba yake. Mwaka jana tuzo ilikwenda kwa Sedat Ergin, wakati bado alipokuwa mhariri mkuu wa gazeti la Uturuki la Harriyet, gazeti la mwisho la kujitegemea lililoweza kumpinga rais Erdogan.
Sherehe ya kupokea tuzo itafanyika katika ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa vyombo vya habari wa Deutsche Welle mjini Bonn tareke 19 mwezi wa June.
Mwandishi: Najma Said
Mhariri: Josephat Charo
www.dw.com/freedomofspeech
www.whca.net
www.dw.com/en