TUNIS:Wahamiaji 35 waokolewa Sfax
15 Mei 2007Polisi wa kushika doria katika pwani za bahari wamewaokoa wahamiaji 35 wa Kiafrika waliojaribu kuingia nchini Italia kupitia pwani ya Libya.Kundi hilo lilirejeshwa katika bandari iliyo eneo la kusini la Sfax Ijumaa iliyopita baaada ya wavuvi wa Tunisia kuwaarifu polisi hao.
Kulingana na gazeti la Assabeh Al Ousboui wahamiaji hao walijaribu kuingia katika kisiwa cha Lampedusa kilicho katikati ya pwani ya Tunisia na kisiwa cha Malta.
Eneo hilo hutumika sana na wahamiaji haramu kuingia barani Ulaya wanaojaribu kuingia katika nchi za Uhispania au Italia.Kwa mujibu wa maafisa wa serikali hali nzuri ya anga inayosababisha bahari kutulia inachangia katika ongezeko la ghafla la idadi ya wahamiaji wanaojaribu kuingia Uhispania kutoka barani Afrika.