Polisi yawatawanya waandamanaji weusi nje ya ofisi za UNHCR
12 Aprili 2023Wahamiaji hao kutoka mataifa ya Afrika Kusini mwa Jagwa la Sahara, waliweka kambi nje ya ofisi za Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR mjini Tunis kwa siku kadhaa, wakisema "hawapo salama" nchini humo.Shirika la habari la AFP lilishuhudia polisi ikizisambaratisha kambi hizo.
Mapema mwezi huu UNHCR ilitangaza inasitisha shughuli za uhifadhi duniani kote wakati ikihamia katika mfumo mpya wa usajili wa wakimbizi.
Famoussa Koita, raia wa Mali ambaye anatambuliwa na Umoja wa Mataifa kama mdai halali wa hifadhi, amesema wamekuwa wakisubiri kwa takriban miaka 2 hadi 3 kwa shirika hilo kukamilisha mchakato wake.
Soma pia:Wahamiaji wa Kiafrika nchini Tunisia bado wakabiliwa na hali ngumu ya kukosa makaazi
Hata hivyo kutokana na matamshi ya Rais Kais mwezi Februari yamewaweka wahamiaji wengi kwenye mashaka.
"kutokana na kile ninachokiona hapa chochote kinaweza kutokea wakati wowote" Faki aliwaambia waandishi wa habari.
Aliongeza kwamba aliwaambia maafisa wa UNHCR kutoka nje na kuzungumza na waandamanaji lakini ilikuwa tofauti.
"UNHCR walijaribu lakini watu hawakuwaelewa." Alisema muhamiaji huyo ambae hadi sasa nae hajui mustakabali wake.
Tunisia:Polisi imetekeleza ombi la UNHCR
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani wa Tunisia Faker Bouzghaya amesema polisi waliingilia kati kufuatia ombi la UNHCR na hadi sasa tayari waandamanaji takriban 80 wanazuiliwa na mamalaka.
Mamia ya waandamanaji waliweka kambi nje ya UNHCR iliyo karibu ya Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, bila kupata huduma ya vyoo au maji safi.
Tangu Saied alipodai bila ushahidi mwezi Februari kwamba wahamiaji kutoka Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara wanasababisha uhalifu na waliwakilisha "njama" ya mabadiliko ya kile alichokiita Muundo wa idadi ya watu wa Tunisia ambao ni waarabu, wahamiaji hao wameendelea kusaka haki ya kuondolewa nchini humo.
Muda mfupi baada ya hotuba yake, Waafrika weusi walikabiliwa na wimbi la ghasia na wengi wakiwemo wanawake wajawazito na watoto.
Soma pia:Mamia ya wahamiaji wa Kiafrika wenye hofu waikimbia Tunisia
Walifukuzwa kutoka kwenye nyumba zao na maeneo ya kazi na wamiliki wa nyumba na waajiri wakihofia kutozwa faini au kufungwa jela.
Baadhi ya wahamiaji wamewaambia waandishi wa habari kwamba wamefukunzwa kwenye nyumba walizopanga na hata ajira zao isivyo haki.
Mamia ya waafrika magharibi waliojawa na hofu walirejeshwa kwenye mataifa yao kwa ndege maalum, punde tu baada ya hotuba ya rais Kais.
Jumuiya ya Kimataifa ililaani vikali matamshi ya Saed kwa kile ilichokiita kuanzisha mashambulizi na wimbi la mitizamo ya chuki nchini humo.
Mashirika ya haki za binadamu nayo yalisema mamia ya wahamiaji wameripoti kushambuliwa na kunyanyaswa isivyo kawaida.