1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

'Tunahitaji siasa zenye miiko na maadili'

5 Mei 2017

Mwanasheria maarufu PLO Lumumba kutoka Kenya ambaye anasifika kwa kupinga vikali ufisadi na kukosoa tawala za Afrika anawataka Waafrika wachukue hatua za dhati kubadili hali ya utawala duni katika nchi zao.

https://p.dw.com/p/2cTxw
Patrick Loch Otieno Lumumba katika mahojiano na DW
Picha: DW/L. Emmanuel

Q AND A WITH PLO LUMUMBA fin J1 SAT LUBEGA - MP3-Stereo

Katika mahojiano maalumu na mwandishi wetu Lubega Emmanuel mjini Kampala, Uganda, kwenye fukwe za ziwa Victoria baada ya kutoa mhadhara wa kufunga kongamano la wataalamu wa uhasibu, Lumumba, aliyewahi kuwa mkurugenzi wa kupambana na rushwa Kenya. amekariri mwito wake wa mageuzi kabambe kufanyika kuhusiana na uongozi na suala zima la demokrasia barani Afrika ili kukabiliana na mdororo wa uchumi na maendeleo ya kijamii. Ameanza kwa kuelezea tatizo kuu la bara Afrika.