1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tume ya uchaguzi Kongo yafuta matokeo ya wagombea ubunge 82

6 Januari 2024

CENI imetangaza kuufuta uchaguzi kwenye majimbo mawili ya uchaguzi nchini humo kufuatia kile imesema ni kupatikana kwa ushahidi wa kutosha kwamba sheria za uchaguzi zilikiukwa.

https://p.dw.com/p/4avKR
Tume ya Uchaguzi Kongo CENI yafuta uchaguzi katika majimbo mawili ya uchaguzi
Tume ya Uchaguzi Kongo CENI yafuta uchaguzi katika majimbo mawili ya uchaguziPicha: ARSENE MPIANA/AFP

Tume ya uchaguzi Kongo CENI imesema imechukua uamuzi huo baada ya ripoti ya uchunguzi iliyoufanya kuonesha baadhi ya wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani kwenye majimbo hayo  walishiriki kufanya vitendo vya udanganyifu.

Msemaji wa tume ya uchaguzi Kongo, Patricia Nseya, amesema wabunge wateule 82 akiwemo gavana wa mji wa Kinshasa na mawaziri wa nne wa serikali wamefutwa katika orodha ya wagombea kutokana na kuhusishwa na vitendo vya rushwa, wizi wa kura na kushikilia kinyume cha sheria vifaa vya kielektroniki vya kupigia kura.

Huku hayo yakijiri, mahakama ya Katiba nchini Kongo inatarajiwa kusikiliza kesi iliyowasilishwa na mgombea huru wa Urais Theodore Ngoy ya kupinga uchaguzi huo wa Desemba 20. Upinzani umekuwa ukiomba uchaguzi huo urudiwe.