1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tulia, Spika mpya wabunge la Tanzania

Admin.WagnerD1 Februari 2022

Aliyekuwa naibu Spika wa bunge la Tanzania Tulia Ackson amechaguliwa kuwa Spika wa bunge hilo  baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa nafasi hiyo muhimu ya moja ya mihimili ya serikali ya Tanzania.

https://p.dw.com/p/46Nj5
Tansania Dr. Tulia Ackson
Picha: Ericky Boniphace

Tulia amechaguliwa kushika nafasi hiyo baada ya aliyekuwa Spika wa bunge hilo, Job Ndugai, kutangaza kujiuzulu mapema mwanzoni mwa mwezi wa kwanza kufuatia kutofautiana kauli na Rais wa nchi hiyo Samia Suluhu Hassan.

Tulia ambaye ni mbunge wa Mbeya Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi CCM alikuwa ni miongoni wa wagombea Tisa waliojitokeza kugombea nafasi hiyo,ambapo yeye pekee alikuwa anatoka bungeni na wagombea 8 wametoka nje ya bunge wakiwakilisha vyama vingine vya siasa.

Safari ya Dr Tulia ilianzia kwenye mchakato ndani ya chama ambapo alikuwa miongoni mwa wagombea 71 waliochukua na kurudisha fomu za kuwania nafasi hiyo na Januari 20 kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM kupitisha jina lake pekee kuwa mgombea wa nafasi hiyo kwa tiketi ya CCM.

Sikiliza Mahojiano: 

Dr. Tulia Ackson wa CCM kuwania uspika wa Tanzania

Awali akiomba kura kwa wajumbe wa mkutano huo wa uchaguzi Tulia Ackson alisema kuwa atahakikisha kuwa bunge atakaloliongoza litakuwa lenye haki licha ya kuwepo na mtizamo tofauti kutoka kwa watu mbalimbali kuwa mbunge hilo limekuwa la chama kimoja.

Tulia Ackson amechaguliwa kwa kura 376 kutoka kwa wabunge wa bunge la Tanzania.

Deo Kaji- Dodoma