1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tulia Ackson wa Tanzania achaguliwa spika wa IPU

27 Oktoba 2023

Spika wa Bunge la Tanzania Tulia Ackson amechaguliwa kuwa rais wa 31 wa Umoja wa Mabunge Duniani, IPU, katika kikao cha Baraza la Uongozi wa muungano huo kilichofanyika mjini Luanda, nchini Angola hii leo.

https://p.dw.com/p/4Y8CO
Spika wa Bunge la Tanzania Dr. Tulia Ackson
Spika wa Bunge la Tanzania Dr. Tulia Ackson Picha: Ericky Boniphace

Ackson anachukuwa nafasi hiyo kutoka kwa Duarte Pacheco, mbunge kutoka Ureno, ambaye amekamilisha muhula wake wa miaka mitatu katika mkutano wa 147 wa IPU.

Katika kura hiyo ya siri iliyopigwa na wabunge wapatao 700kutoka mataifa 130 ikiwemo wajumbe kutoka mataifa yalioko vitani au katika mazingira ya mizozo, Spika Tulia Ackson aliwashinda wagombea wengine watatu kwa kupata asilimia 57 ya kura katika duru ya kwanza y aupigaji kura.

Soma pia:Spika wa Tanzania achaguliwa kuwa rais wa Mabunge duniani

Ili kuhimiza usawa wa kijinsia, kila bunge mwanachama wa IPU lilipewa kura tatu kwa sharti la kuwa na ujumbe wenye usawa wa kijinsia, huku ujumbe wenye jinsia moja tu ukipewa kura moja.