Tshisekedi asema anataka kuzungumza na Rwanda na siyo M23
23 Februari 2024Vikosi vya jeshi la Kongo, FARDC, Wazalendo, na vikosi vingine vinavyoiunga mkono serikali vilipambana haraka, kuzuia jaribio hilo.
Mapigano hayo yaliendelea hadi saa moja asubuhi na kusababisha majeruhi wanne na vifo vya watu watatu, wakiwemo watoto wawili, kulingana na vyanzo vya eneo hilo.
Ijumaa asubuhi utulivu kiasi ulionekana kurejea katika mji wa Sake, ambao bado uko chini ya udhibiti wa jeshi la taifa FARDC na wapiganaji wazalendo.
Katika hotuba yake kwa taifa Alhamisi usiku, Rais wa DR Kongo Felix Tshisekedi alikariri tuhuma zake kwamba Rwanda inajificha ya kundi la M23, na kuongeza kuwa hiyo ndiyo sababu hawezi kuzungumza na kundi hilo.
"Mazungumzo ningependa kufanya tu na Rwanda kwa sababu wao ndio walionishambulia. Nilimwambia Paul Kagame huko Addis Ababa kwamba ni ninyi niliopenda kuzungumza nanyi na kuwauliza: Mnapenda nini kwa nchi yangu na watu wangu?" alisema Tshisekedi.
Rais wa Jamhuri alitaka kwa njia hii kuwahakikishia watu kwamba anafanya kila awezalo kutafuta amani mashariki mwa nchi yake.
Soma pia: Raia wakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula Goma
Maneno haya yanaonekana kama matamko hewa wakati Umoja wa Ulaya ambao umeingia mkataba wa madini na Rwanda, unaendelea kuishi kwa amani nchini DRC. Hii ni kulingana na Jack Sinzahera, mwanaharakati wa haki za binadamu.
"Ni ajabu kwamba kuna mzozo kati ya Rwanda na Kongo, na muungano wa Ulaya unaingia mkataba wa madini na Rwanda, ingawa madini hayo ambayo Rwanda inazalisha mengi yanajulikana kama madini ya damu. Viongozi wetu wa Kongo wanapaswa kuwa serious katika mambo haya ya madini."
M23 wazidisha mashambulizi Sake
Wakati rais Tshisekedi akizungumza juu ya hali ya usalama mashariki mwa nchi yake, waasi wa M23 walizidisha mashambulizi yao katika mji wa Sake ambao umekimbiwa na wakaazi.
Soma pia: Rwanda yatupilia mbali wito wa Marekani jeshi Kongo
Mashambulizi haya yalisababisha vifo vya watu watatu wasio na hatia na kujeruhi raia wanne. Kwa Jean Baptiste Kasekwa mwanasiasa na mchambuzi nchini kongo, Felix Tshisekedi anapaswa kutoa risasi kwa vikosi vilivyounganishwa vya DRC.
"Rwanda inaendelea kuua watu kupitia M23 watu ambao waliuawa Sake. Watu wengi wamekuwa wakimbizi. Juzi ilikuwa vita Kashuga, leo M23 Rwanda Uganda wanafanya vita huko Kihondo karibu na Nyanzale, Tunatake, kama ana nia halisi ya kupambana na Rwanda, kama hayupo katika uhusiano na adui, a ruhusu na apane vifaa vya vita kwa askari na Wazalendo, kiasi kwamba wafungue vita kwa njia zote," alisema Kasekwa.