Tshisekedi amteuwa Tuluka kuwa waziri mkuu
2 Aprili 2024Suminwa, aliyekuwa waziri wa mipango, ni mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa wa waziri mkuu nchini humo.
Uteuzi wa Suminwa unahitimisha wiki kadhaa zilizogubikwa na hali ya suintofahamu kuhusu wadhifa huo.
Katika hotuba yake kupitia televisheni ya taifa, Suminwa alisema anafahamu kuhusu jukumu kubwa linalomkabili na kwamba angelifanya kazi kuhakikisha uwepo wa amani na maendeleo nchini Kongo.
Soma zaidi: Tshisekedi amteuwa Judith Suminwa kuwa waziri mkuu Kongo
Kuapishwa kwa Tshisekedi kwa muhula wa pili madarakani mnamo mwezi Januari, kulianzisha mchakato wa muda mrefu wa kutafuta muungano wa vyama vingi katika bunge la kitaifa, hatua muhimu kabla ya kuteuliwa kwa waziri mkuu na kuundwa kwa serikali mpya.
Serikali mjini Kinshasa inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na mgogoro unaozidi kutanuka katika maeneo ya Mashariki mwa nchi hiyo.