Trump na Biden washambuliana katika kampeni Florida
30 Oktoba 2020Huku uchaguzi nchini humo utakaofanyika Jumanne ukikaribia maelfu ya watu wengi wao wakiwa bila barakoa walikusanyika katika mkutano wa Rais Trump ambapo kiongozi huyo alimkejeli mpinzani wake.
"Hebu fikiria, nipoteze uchaguzi kwa mtu huyu? inawezekana kweli?" alisema Trump.
Rais huyo wa Marekani ameendelea kupuuza janga la Covid 19 akiwaambia wafuasi wake kwamba hata watakapoambukizwa, watapona tu kama alivyopona yeye baada ya kuambukizwa.
Trump amefanya tukio kubwa la kusambaza virusi vya corona
Masaa machache baadae Biden aliwasili katika eneo hilo kuwahutubiawafuasi wake waliokuwa ndani au karibu ya magari yao wakiwa wamevaa barakoa kwa ajili ya kupunguza kusambaa kwa virusi hivyo, ingawa hakukuwa na umbali wa mtu hadi mtu kila wakati.
Biden amemkosoa Trump kwa kufanya kile alichokiita ni "tukio kubwa la kusambaza virusi vya corona" na akashambulia matamshi ya kila mara ya rais huyo kwamba Marekani imevuka kipindi kibaya cha janga la virusi vya corona, licha ya ongezeko la maambukizi kote duniani.
"Donald Trump ameipeperusha bendera nyeupe, ameziacha familia zetu na kushindwa kukabiliana na virusi vya corona," alisema Biden. "Ila Wamarekani hawafi moyo, hatutofi moyo," aliongeza mgombea huyo wa Republican.
Janga la Covid-19 limesababisha maafa mengi Marekani ambapo kufikia sasa zaidi ya watu 227,000 wamefariki dunia. Fauka ya hayo mamilioni ya watu wamepoteza kazi.
Jopokazi la White House linaonya kuhusiana na mwendeleo wa maambukizi ya virusi vya corona kwa kiwango kikubwa, ikiwemo katika majimbo ambayo yatakuwa ni muhimu mno katika uchaguzi.
Jimbo la Florida ni muhimu kwa uchaguzi wa Marekani, Jumanne
Rais Donald Trump amekuwa na kipindi ratiba ya kampeni yenye shughulichungunzima ambapo wakati mwengine alikuwa akifanya hata mikutano mitatu katika majimbo tofauti kwa siku moja. Biden kwa upande wake amekuwa akifanya mambo kwa uangalifu mkubwa, kama wiki hii amekuwa katika jimbo lake la nyumbani la Delaware kwa siku mbili nzima.
Jimbo la Florida ni muhimu sana kwa uchaguzi huo wa Jumanne kwani ushindi wa Trump katika jimbo hilo mwaka 2016 ulichangia pakubwa yeye kuibuka mshindi wa urais.
Ila kwa sasa kura za maoni zinamuonyesha Biden akiwa anaongoza kote nchini humo, lakini anamzidi Trump kwa alama chache tu katika majimbo muhimu.
Kura ya maoni ya shirika la Ipsos kwa ushirikiano na shirika la habari la Reuters iliyofanywa Jumatano, inaonyesha kuwa Trump anakaribiana na Biden katika jimbo la Florida. Kura hiyo inamuonyesha Trump akiwa na asilimia 47 ikilinganishwa na asilimia 49 yake Biden.