Trump aondosha wanajeshi majimboni
30 Julai 2020Gavana wa mji wa Oregon, Kate Brown, alisema majeshi ambayo uwekwaji wake ulionekana na wengi kama sehemu ya kaulimbiu mpya ya Rais Donald Trump ya "amani na sheria", ambayo inahusishwa na kampeni za kutaka kuchaguliwa tena kwenye uchaguzi wa Novemba, wataanza kuondolewa kwa awamu kuanzia leo (Julai 30).
Hata hivyo, Kaimu Waziri wa Usalama wa Ndani, Chad Wolf, aliashiria kuwa wanajeshi hao wataondolewa iwapo tu kutakuwa na uhakikisho kuwa polisi wa mji huo watahakikisha jengo la Mahakama ya Juu ya Shirikisho litakuwa salama.
Mapema mwezi juu, utawala wa Trump ulituma wanajeshi kuingilia kati katika mji huo, baada ya wiki kadhaa za maandamano dhidi ya ubaguzi na ukatili wa polisi kwa Wamarekani wenye asili ya Afrika, ambazo zilishuhudia madirisha yakivunjwa na jengo la Mahakama ya Juu ya Shirikisho na majengo mengine kuchafuliwa kwa rangi.