Trump akosolewa kwa kuashiria kuzitwaa Greenland, Canada
8 Januari 2025Akizungumza na waandishi wa habari mjini Fllorida hapo jana, alisema hawezi kuondosha uwezekano wa kutumia nguvu za kiuchumi au kijeshi kutwaa udhibiti wa Mfereji wa Panama na Greenland.
Kwa upande mwengine, Trump alikosowa vikali utumiaji wa bidhaa za Canada na pia msaada wa kijeshi wa Marekani kwa jirani yake huyo, akidai mpaka baina yao ni wa kubuni.
Soma zaidi: Trump bado anakabiliwa na hukumu ya kumlipa kahaba
Kuhusu Greenland, kisiwa chenye utajiri wa rasilimali kinachomilikiwa na Denmark, Trump alisema atatumia shinikizo la kiuchumi ikiwa Copenhagen itakataa kuiuzia Marekani kisiwa hicho.
Waziri Mkuu wa Canada, Justin Treudau, amemkosowa vikali Trump kwa kauli yake hiyo, huku Panama ikisema hakuna namna yoyote ambapo itayatowa mamlaka yake kwa Marekani.
Waziri Mkuu wa Denmark, Mette Frederiksen, amesema kisiwa cha Greenland hakiko kwenye mnada.