Trump akabiliwa na mashitaka mapya kuhusu uchaguzi wa 2020
28 Agosti 2024Waendesha mashtaka nchini Marekani wamewasilisha mashtaka mapya dhidi ya rais wa zamani Donald Trump. Mashtaka hayo yamewasilishwa kujibu hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Juu ya Marekani iliyosema kwamba marais wa Marekani kwa jumla wanayo stahiki ya kinga dhidi ya kushtakiwa kwa makosa ya uhalifu wanapokuwamo madarakani.Trump kurejea kortini tena Jumanne baada ya siku ya kwanza ya kesi ya jinai dhidi yake
Mashtaka hayo manne yaliyopitiwa upya yanamuhusu Trump ambaye sasa ni mgombea urais na siyo kama rais aliyemo madarakani. Kwa mujibu wa mashtaka hayo Trump anatuhumiwa kujaribu kuingilia kati matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020 ambapo alishindwa na Rais Joe Biden.
Mawakili wa Trump wamekuwa wakijaribu kuchelewesha kesi hadi baada ya uchaguzi wa Novemba atakapochuana na makamu wa rais Kamala Harris, mgombea wa chama cha Democratic. Trump pia anakabiliwa na mashtaka huko Georgia kuhusiana na juhudi za kupindua uchaguzi wa 2020.