Trump agoma kurudi mahakamani
11 Desemba 2023Matangazo
Akiandika kwenye mtandao wake wa kijamii uitwao Truth Social, bilionea huyo anayetaka kuteuliwa na chama chake cha Republican kuwania tena urais mwakani, amesema ameshatowa ushahidi wa kutosha na hana cha kuongeza.
Soma zaidi: Donald Trump anakabiliwa na msururu wa kesi za uhalifu, lakini anakana kufanya kosa lolote
Trump alikuwa anatakiwa kuhudhuria kikao chengine cha mahakama siku ya Jumatatu (Disemba 11) kwenye kesi iliyofunguliwa dhidi yake na Mwanasheria Mkuu wa New York, Letitia James.
Mwanasheria huyo anamtuhumu Trump kwa kutia chumvi kwenye taarifa zake za kifedha ili kujipatia mikopo na mikataba ya biashara.
Kesi hiyo inatishia kuiporomosha biashara ya ujenzi ya Trump na kuiharibu taswira yake kama mfanyabiashara aliyefanikiwa.