Trump afanya uchaguzi wa kwanza wa baraza la mawaziri
8 Novemba 2024Rais mteule wa Marekani Donald Trump jana alifanya uteuzi wake wa kwanza wa baraza la mawaziri baada ya ushindi wake katika uchaguzi wa urais, huku akiashiria nia yake ya kuachana na sera ya utawala unaomaliza muda wake kwa kuzungumza na rais wa Urusi Vladimir Putin. Biden awataka Wamarekani "kutuliza joto la kisiasa"
Msimamizi wa kampeni za Trump Susie Wiles atahudumu kama mkuu wa utumishi wa Ikulu ya White House, akiwa mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huo na mteule wa kwanza wa chama Republican katika utawala huo mpya unaoingia madarakani.
Wengine wanaotarajiwa kuwa katika mstari wa mbele kujinyakulia nyadhifa katika utawala huo wa Trump ni pamoja na Robert F. Kennedy Jr, kiongozi mkuu katika vuguvugu la kupinga chanjo ambaye Trump ameahidi kumpa jukumu kubwa katika sekta ya huduma ya afya na tajiri mkubwa zaidi duniani Elon Musk, hali inayoakisi sura ya kutatanisha ambayo huenda utawala huo ukachukuwa.