1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Togo yaimarisha udhibiti wa Covid baada ya vifo vya mahujaji

29 Juni 2024

Togo imekuwa nchi ya pili ya Afrika Magharibi kutekeleza vipimo vya uchunguzi wa Covid na uvaaji wa barakoa kwa mahujaji wanaorejea kutoka katika ibada ya hija ya mwaka huu Waislamu huko Makka.

https://p.dw.com/p/4hf3m
Saudi Arabia Mecca Hajj joto
Wahudumu wa afya wakiwa wamembeba muhujaji kwa uchunguzi wa afya yake baada ya kuanguka kutokana na joto huko Mina, karibu na mji mtakatifu wa Makka, Saudi Arabia, Juni 16, 2024.Picha: Rafiq Maqbool/AP Photo/picture alliance

Senegal ndio ilikuwa nchi ya kwanza katika kanda hiyo kutekeleza vipimo vya hiari, ikishuku kuwa idadi ya vifo 1,300 ikiwa ni kwa mujibu wa Saudi Arabia vifo vyao vilitokana na ugonjwa wa kupumua kama vile Covid-19.

Taarifa ya jana Ijumaa ya serikali ya Togo imesema mahujaji wanaorejeawatalazimika kufanyiwa vipimo vya lazima vya Covid na kuzuiwa kukutana na watu, kuvaa barakoa na kuepuka mikusanyiko mikubwa" kwa siku 10 baada ya kurejea.

Takriban asilimia 18 ya raia milioni nane wa Togo ni Waislamu. Kwa mwaka huu, raia wa Togo wapatao 2,500 walienda Saudi Arabia kwa ajili ya ibada ya hija, ikiwa moja kati ya nguzo tano kwa waumnini wa dini ya Kiislamu.