Takwimu za shirika la Ujerumani la kuhifadhi matumizi ya data za mitandaoni zinaonyesha kuwa zaidi ya watu bilioni 4 duniani kote wanatumia mitandao ya kijamii. Tafsiri yake ni kwamba, mitandao ya kijamii imechukua sehemu kubwa ya maisha ya watu hasa vijana. Kwenye Kurunzi Live, tunajadili kuhusu sura za watu mitandaoni. Je, unaweza kutofautisha vipi kati ya maisha ya mtu mtandaoni na uhalisia?