1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu ya wanamichezo wakimbizi katika Olimpiki

4 Juni 2016

Kamati ya kimataifa ya Olimpiki – IOC imezindua timu yake ya kwanza kabisa ya wakimbizi itakayokuwa na wanamichezo 10 na maafisa 12 na itashindana katika Michezo ya Olimpiki ya Rio 2016 chini ya bendera ya Olimpiki

https://p.dw.com/p/1J0ah
Thomas Bach Präsident Internationales Olympisches Komitee
Picha: picture-alliance/dpa/L. Gillieron

Katika kile Rais wa IOC Thomas Bach amekiita kuwa ni “siku ya kihistoria”, kikosi hicho kinawajumuisha wanamichezo watano kutoka Sudan Kusini, wawili kutoka Syria, wawili kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia na mmoja kutoka Ethiopia. Wamamichezo hao walichaguliwa kutoka kikosi cha wakimbizi 43.

Bach amesema "Tuna hakika kuwa timu hii ya wakimbizi katika Olimpiki inaweza kuwa idhara ya matumaini. Ishara ya matumaini kwa wakimbizi wote ulimwenguni na inaweza kutuma ujumbe kwa jamii ya kimataifa kuwa wakimbizi ni binadamu wenzetu na muhimu katika jamii. Wanamichezo hawa wakimbizi wataonyesha ulimwengu kuwa licha ya mikasa mikubwa waliyopitia, yeyote anaweza kuchangia katika jamii kupitia vipaji vyao, ujuzi na nguvu za roho ya kibinaadamu"

IOC itaipa timu hiyo ya wakimbizi sare za michezo na kuwapa makocha na maafisa wa timu.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu