1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Thailand yashiriki uchaguzi wa bunge

14 Mei 2023

Wapiga kura wa Thailand leo wanapiga kura katika uchaguzi uliotajwa kuwa nafasi muhimu ya mabadiliko, miaka minane baada ya Waziri Mkuu Prayuth Chan-ocha kuingia madarakani kufuatia mapinduzi ya 2014.

https://p.dw.com/p/4RKDl
Thailand Bangkok | Parlamentswahl
Picha: Lillian Suwanrumpha/AFP/Getty Images

Anakabiliana na binti wa mwanasiasa ambaye haungwi mkono na jeshi la nchi hiyo.Chama cha upinzani cha Pheu Thai, kinachoongozwa na Paetongtarn Shinawatra, kwa kiwango kikibwa kinatabiriwa sana kushinda kiwango fulani cha wingi wa viti vya unge katika bunge la viti 500.Baada ya kupiga kura yake, Paetongtarn alisema kila kura ni muhimu kwa kuleta mabadiliko nchini Thailand na kwamba ana matumaini makubwa kwa matokeo ya mwisho. Waziri Mkuu Prayuth analaumiwa kwa uchumi unaodumaa, mapungufu katika kushughulikia janga la UVIKO-19, na kuzuia mageuzi ya kidemokrasia, jambo ambalo limekuwa likipiganiwa na wapiga kura vijana.