1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Thailand yaanza kupeleka misaada nchini Myanmar

25 Machi 2024

Thailand imeanza kuwasilisha msaada kwa Myanmar inayotawaliwa na wanajeshi katika mpango wa msaada wa kibinadamu kwa lengo la kufungua njia ya kufanyika mazungumzo kati ya kambi zinazopingana.

https://p.dw.com/p/4e5xQ
Myanmar | wanajeshi
Myanmar imekosa utulivu kwa miaka mitatu ya vurugu zilizochochewa na mapinduzi.Picha: Hkun Lat/Getty Images

Wizara ya mambo ya nje ya Thailand imesema katika taarifa yake kwamba shehena ya kwanza la mifuko 4,000 ya mchele na bidhaa nyingine muhimu kwa watu wapatao 20,000 vimepelekwa nchini Myanmar na Shirika la Msalaba Mwekundu la Thailand kupitia kwenye kivuko cha mpaka cha Mae Sot-Myawaddy.

UN yasikitishwa na mashambulizi ya anga yanayoendelea Myanmar
Mradi huo wa amani wa Thailand unaungwa mkono na wanachama 10 waJumuiya ya Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN).

Umoja wa Mataifa umesema takriban watu milioni 2.6 wayamekimbia makazi yao kutokana na mapigano na zaidi ya watu milioni 18 wanahitaji msaada.