1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tetemeko la 5.3 lazikumba Pakistan na Kashmir

20 Agosti 2024

Tetemeko la ardhi la kipimo cha 5.3 limezikumba sehemu za Himalaya kwenye jimbo la Kashmir la upande wa Pakistan.

https://p.dw.com/p/4jgB2
India | Jimbo la Kashmir
Moja ya maeneo ya milimani ya eneo la Kashmir. Baadhi ya maeneo ya kusini yamekumbwa na tetemeko la ardhiPicha: DW

Maafisa wa idara husika wamesema hakuna madhara yaliyotokea. Kitovu cha mitetemeko kilikuwa kwenye sehemu ya kusini magharibi mwa jimbo la Kashmir linalozitenganisha India na Pakistan.

Kwa mujibu wa taarifa ya kituo cha kitaifa kinachofuatilia mitetemeko ya ardhi, kina cha mitetemeko kilifikia kilometa 20 na sehemu mbalimbali za Pakistan ikiwa pamoja na mji mkuu Islamabad zilikumbwa na mitetemeko. 

Mnamo mwaka 2005 tetemeko la ukubwa wa 7.6 lilisababisha vifo vya maalfu ya watu nchini Pakistan na kwenye jimbo la Kashmir.