1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ten Hag: Carabao ni motisha wa makombe zaidi

27 Februari 2023

Kocha wa Manchester United huko England, Erik Ten Hag anasema kwa sasa klabu hiyo inaelekeza macho kwenye mechi ya Jumatano watakapopambana na West Ham United katika mashindano ya FA Cup.

https://p.dw.com/p/4O1ue
Fußball I Erik ten Hag
Picha: Zac Goodwin/empics/picture alliance

Ten Hag anasema ni sharti washerehekee ushindi wao wa 2-0 dhidi ya Newcastle United katika kombe la Carabao katika uwanja wa Wembley ila wasisahau kwamba msimu bado haujaisha.

"Kwa mtazamo wetu, kila mechi ni muhimu na huezi kushinda kama hauko imara kwa asilimia 100. Kwa hiyo tuanstahili kufanya kila tuwezalo kushinda mechi hii. Ila kombe hili linaweza kuwa motisha wa kushinda zaidi na kuwa pamoja zaidi na kuweka juhudi zaidi pamoja kwasababu hatutatosheka," alisema Ten Hag.

Fußball I Manchester United v Arsenal - Premier League - Old Trafford
Wachezaji wa Manchester United Marcus Rashford na AntonyPicha: Martin Rickett/empics/picture alliance

Kombe hilo la Carabo waliloshinda United lilikuwa lao la kwanza katika kipindi cha miaka sita.

Kwa upande wao wachezaji wa Newcastle United wanasema wamevunjwa moyo na kushindwa kwao jana ila hawana budi kutazama mbele kwani wanahisi walicheza vyema na walikuwa katika kiwango sawa na hao wapinzani wao. Kieran trippier ni beki wa kulia wa Newcastle United.

"Tunajiamini sana katika timu hii, tuna umoja sana katika kundi hili na yote haya yanatoka kwa kocha, Na kama nilivyosema, unajua wakati kama huu mwaka jana, tulikuwa tunapambana tusishushwe daraja. Sasa tumefika fainali ya kombe la ligi kwa hiyo tumepiga hatua kubwa sana," alisema Trippier.