1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Mwanadiplomasia wa Iran alishutumu shirika la CIA

7 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCBi

Mwanadiplomasia wa Iran aliyeachiliwa huru baada ya kukamatwa miezi miwili iliyopita nchini Irak, amelishutumu shirika la ujasusi la Marekani, CIA, kwa kumtesa wakati alipokuwa akizuiliwa.

Televisheni ya taifa nchini Iran imetangaza kwamba Jalal Sharafi amesema shirika la CIA lilimhoji kuhusu uhusiano baina ya Iran na Irak na misaada kwa makundi kadhaa.

Sharafi amesema alipoeleza kwamba Iran ina uhusiano rasmi wa kawaida na Irak, aliteswa zaidi usiku na mchana kutumia mbinu tofauti.

Mwanadiplomasia huyo alikamatwa mnamo tarehe 4 mwezi Februari na watu waliokuwa na bunduki katika wilaya ya Karradah inayomilikiwa na Washia mjini Baghdad.

Aliachiliwa huru Jumanne iliyopita.