TEHRAN : Mkutano wa Maangamizi ya Wayahudi waendelea
12 Desemba 2006Mkutano tata wa kuhoji ukweli juu Maangamizi ya Wayahudi wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia unaofanyika mjini Tehran leo umeingia siku ya pili na ya mwisho.
Israel,Marekani na spika wa bunge la Ujerumani wameulani mkutano huo.Katika kuupinga mkutano huo serikali ya Ujerumani imekuwa ikifanya mkutano mwengine wa wataalamu dhidi ya mkutano huo wa Iran.Mtafiti mwandamizi wa Ujerumani katika masuala ya chuki dhidi ya Wayahudi Wolfgang Benz amesema matukio ya sera kali za mrengo wa kulia yanazidi kupata nguvu katika kujinadi.
Ni uhalifu kukana Maangamizi ya Wayahudi katika nchi kadhaa za Ulaya ikewemo Ujerumani na Austria.
Rais Mahmoud Ahmedinejad wa Iran mara kadhaa ameelezea mashaka yake juu ya kutokea kwa mauaji hayo ya Wayahudi milioni sita wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.