SiasaMali
Tawala za kijeshi Afrika magharibi, zataka zirudishwe ECOWAS
10 Februari 2023Matangazo
Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa jana mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa ya Mali, Guinea na Burkina Faso wamesema wamefikia makubaliano ya kufanya kazi pamoja kufanikisha kurejeshwa kwa mataifa hayo kuwa wanachama wa Umoja wa Afrika na jumuiya ya kiuchumi ya ECOWAS.
Uanachama wa nchi hizo tatu ndani ya ECOWAS na Umoja wa Afrika ulisitishwa kwa nyakati tofauti kutokana na mapinduzi ya kijeshi yaliyokosolewa vikali.
Taasisi hizo mbili zinataka tawala za kiraia kurejea madarakani kama sehemu ya masharti ya kuondoa kikamilifu vikwazo na vizuizi dhidi ya mataifa hayo matatu.