Tanzania yazindua Mgodi rasmi wa madini
21 Agosti 2014Matangazo
Hatua hiyo imechukuliwa na serikali kama juhudi za kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa watanzania.Aidha waziri wa nishati na madini nchini humo Sospeter Muhongo amesema mgodi huo wa dhahabu wa Biharamulo utafuatiwa na mingine kadhaa itakayotowa pia nafasi za ajira kwa wazawa ingawa amesisitiza Tanzania haina nia ya kuwafukuza wageni wanaosimamia migodi mingine ya nchi hiyo . Saumu Mwasimba amezungumza nae mchana huu na kutupa maelezo kamili kuhusu mgodi huo na hatua hiyo ya serikali. Kuskiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Saumu Yusuf
Mhariri: Josephat Charo