Serikali ya Tanzania imesema hakutakuwa na huruma kwa watu wote wanaojihusisha na matukio ya kihalifu na kwamba vyombo vya ulinzi vimejipanga kukabiliana na vitendo hivyo. Hii ni baada ya kuripotiwa kwa matukio kadhaa ya vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na kundi linalojiita "Panya Road." Sikiliza ripoti ya Deo Kaji Makomba kutoka Dodoma.