1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tamasha la Kanivali lakamilika

15 Februari 2010

Kilele cha kanivali kilifikiwa leo, jumatatu ya mawaridi, katika miji kadhaa ya hapa Ujerumani inayopakana na Mto mkubwa wa Rhein; watu wakiwa hawaijali baridi kali, theluji na barafu iliotanda.

https://p.dw.com/p/M1wF
Paredi la Karneval,ColognePicha: DW

Katika jiji la Kolon, watu 11,000, wengi wao wakiwa katika malori yaliofanya paredi hiyo, walirusha peremende na chokoleti kwa karibu watu milioni moja waliosimama mabarabarani za urefu unaopata kilomita saba. Picha ya kubeza ilioonekana katika peredi hiyo ni ile inayomshabihisha Kansela Angela Merkel na mwanamke wa kwaza, Eva, akipokea tunda lilokatazwa kuliwa peponi; ikimaanisha anapokea CD yenye maelezo ya watu waliokwepa kulipa kodi na kuhamisha akiba zao za benki huko Uswissi...