Taliban yaiomba Pakistan kutoa muda zaidi kwa raia kuondoka
1 Novemba 2023Utawala wa Taliban nchini Afghanistan umeiomba Pakistan kuwapa raia wake wasiokuwa na vibali nchini humo, muda zaidi wa kuondoka wakati kukiwa na mkusanyiko mkubwa wa wakimbizi katika maeneo ya mpakani, wanaotoroka kitisho cha kukamatwa na kufukuzwa kwa nguvu nchini humo.
Serikali ya Islamabad imewapa Waafghan milioni 1.7 wanaoishi nchini Pakistan kinyume cha sheriahadi leo Novemba mosi, kuondoka kwa hiari. Hadi sasa zaidi ya watu 130,000 wameondoka Pakistan tangu amri hiyo ilipotolewa mwezi Oktoba.
Tangu Taliban ilipochukua madaraka mwaka 2021, imewaomba Waaghanistan kurejea nyumbani lakini pia ikakosoa hatua ya Pakistan ikisema raia wake wanaadhibiwa kufuatia mvutano uliopo kati ya mataifa hayo mawili na kutaka raia hao kupewa muda zaidi wa kuondoka.