1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Takriban watu milioni moja waliomba hifadhi EU mwaka 2022

23 Februari 2023

Shirika la Umoja wa Ulaya la waomba hifadhi (EUAA), limeripoti kuwa takriban watu milioni moja waliomba hifadhi katika nchi za Ulaya mwaka uliopita.

https://p.dw.com/p/4Nry0
Grenzschutz-Konferenz in Litauen
Picha: Mindaugas Kulbis/dpa/picture alliance

Shirika la Umoja wa Ulaya la waomba hifadhi (EUAA), limeripoti kuwa takriban watu milioni moja waliomba hifadhi katika nchi za Ulaya mwaka uliopita.

Shirika hilo limesema lilipokea maombi ya hifadhi 966,000, hiyo ikiwa ongezeko la zaidi ya asilimia 50 ikilinganishwa na mwaka 2021.

Kulingana na data zilizopo, hiyo ni idadi ya juu zaidi ya waomba hifadhi shirika hilo limerekodi tangu mwaka 2016.

Idadi hiyo inajumuisha walioomba hifadhi pia nchini Norway na Switzerland, mataifa ambayo si wanachama wa Umoja wa Ulaya.

Wasyria na Waafghanistan waliongoza kwenye orodha hiyo, kufuatia misukosuko ya kisiasa na kiusalama kwenye nchi zao.

Wahamiaji kutoka Ukraine wako katika mfumo mwingine tofauti na hivyo wao si sehemu ya takwimu iliyotolewa.