UN: Watu 50,000 waikimbia Myanmar kufuatia mapigano
10 Novemba 2023Mapigano hayo yaliyoanza wiki mbili zilizopita yameendelea katika jimbo la kaskazini la Shan karibu na mpaka wa China, katika kile wachambuzi wanasema kinaleta changamoto kubwa zaidi kwa utawala wa kijeshi tangu uliponyakua mamlaka mwaka 2021.
Kundi linalojiita Muungano wa kidemokrasia wa kitaifa wa jeshi la Myanmar (MNDAA), lile linalojiita Jeshi la Ukombozi la Ta’ang (TNLA) na jingine la Jeshi la Arakan (AA) yamesema yamekamata makumi ya vituo vya kijeshi na kuziba njia muhimu za biashara kuelekea China.
Kiongozi wa Myanmar asema uasi unatishia kulisambaratisha taifa hilo
Kulingana na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu masuala ya kibinadamu (OCHA), kufikia jana Novemba 9, karibu watu 50,000 kaskazini mwa Shan, walilazimika kuyahama makaazi yao.