1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Takriban watu 40 wamekufa katika boti ya wahamiaji Haiti

20 Julai 2024

Takriban watu 40 wamefariki baada ya mashua iliyokuwa imewabeba wahamiaji kushika moto katika pwani ya Haiti, limesema Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM)

https://p.dw.com/p/4iXew
Kolumbien Haitianischen Migranten an der karibischen Küste
Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema watu 40 wamekufa baada ya mashua iliyokuwa imewabeba wahamiaji kushika moto katika pwani ya HaitiPicha: Colombian Navy/AFP

Takriban watu 40 wamefariki baada ya mashua iliyokuwa imewabeba wahamiaji kushika moto katika pwani ya Haiti, limesema Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).

Boti hiyo iliyobeba zaidi ya watu 80, ilishika moto wakati wa safari yake ya kilomita 250 kutoka kaskazini mwa Haiti kuelekea Uturuki. IOM imeongeza kusema kuwa manusura 41 waliokolewa na Walinzi wa Pwani wa Haiti na 11 kati yao wamepelekwa hospitalini kupatiwa matibabu.

Soma zaidi. Kikosi cha kulinda amani Haiti chaahidi kuleta utulivu

Grégoire Goodstein, Mkuu wa misheni wa shirika hilo la uhamiaji amesema "Tukio hili la kusikitisha linaangazia hatari zinazowakabili watoto,wanawake, na wanaume wanaohama kwa njia zisizo za kawaida na ametoa wito wa kusafiri katika njia salama.

Raia wa Haiti wamekuwa wakipitia madhila yanayotokana na ghasia za magenge ya kihalifu. Karibu nusu ya wakaazi milioni 11 wa Haiti wanakabiliwa na njaa huku nusu milioni ya Wahaiti wamegeuka kuwa wakimbizi ndani ya nchi yao.