Takriban watu 15 wameuwawa kwa tetemeko la ardhi Afganistan
7 Oktoba 2023Maafisa katika idara ya kupambana na majanga nchini humo wanasema huenda idadi ya vifo ikaongezeka baada ya ripoti ya maporomoko na waathiriwa kukwama kwenye majengo yalioanguka kufuatia tetemeko hilo.
Soma pia:Tetemeko la ukubwa wa 6.3 lapiga Magharibi mwa Afganistan
Msemaji wa Mamlaka ya Kitaifa ya Kudhibiti Majanga Mullah Jan Sayeq amesema "takriban watu 40 wamejeruhiwa." huku akisisiza kuwa hiyo ni taarifa ya awali huenda idadi ikaongezeka. Huduma muhimu ikiwemo mawasiliano ya simu katika eneo hilo zimetatizika.
Itakumbukwa kuwa, mwezi Juni mwaka uliopita zaidi ya watu 1,000walikufa na maelfu waliachwa bila makaazi baada ya tetemeko la ukubwa wa 5.9 ambalo ni baya zaidi nchini humo kwa kipindi cha robo karne kupiga jimbo masikini la Paktika.