Taiwan yaitaka China kugawana majukumu ili kudumisha amani
1 Januari 2024Wakati wa hotuba yake ya mwaka mpya, Tsai amesema kuwa ''wanatumai kwamba pande hizo mbili zitaanzisha tena mawasiliano thabiti haraka iwezekanavyo'' na kuongeza kuwa Taiwan pia inataka kwa pamoja kutafuta njia kwa pande hizo mbili kuishi kwa pamoja kwa kipindi kirefu kupitia kanuni za "amani, usawa, demokrasia na mazungumzo."
Soma pia: Taiwan yaripoti shughuli zaidi ya kijeshi za China huku uchaguzi ukikaribia
Tsai amesema kuwa chaguo la Taiwan katika siku zijazo bado ni kuendelea kudumisha demokrasia na kulinda amani.
Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Tsai alisema kuwa mustakabali wa uhusiano kati ya Taiwan na China utaamuliwa kwa pamoja na watu wa Taiwan kupitia utaratibu wa kidemokrasia kwa sababu "Taiwan ni nchi ya kidemokrasia.''