1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Tahadhari ya mashambulio ya anga yatolewa kote Ukraine

13 Novemba 2024

Ukraine imetoa tahadhari ya mashambulio ya kutokea angani katika maeneo yote nchini humo.

https://p.dw.com/p/4mwuI
Mzozo wa Urusi na Ukraine
Jeshi la anga la Ukraine lilionya mapema JUmatano kwamba kombora la Urusi lilikuwa linaingia katika anga ya Ukraine kuelekea katika mji mkuu, Kiyv.Picha: SERGEI SUPINSKY/AFP/Getty Images

Tahadhari hiyo imetolewa wakati mkuu wa majeshi akitanabaisha juu ya mashambulio ya makombora kwenye mji mkuu, Kyiv.

Mkuu huyo wa majeshi wa Ukraine amesema Urusi hivi sasa inafanya mashambulio ya makombora katika mji huo.

Jeshi la anga la Ukraine lilionya mapema JUmatano kwamba kombora la Urusi lilikuwa linaingia katika anga ya Ukraine kuelekea katika mji mkuu, Kiyv.

Hujuma hizo zinafuatia mashambulio ya wiki nzima yaliyofanywa na Urusi, ikiwa pamoja na shambulio lililofanyika kwenye mji wa rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky.

Wakati huo huo Rais Zelensky ameonya kuwa Urusi imetayarisha kikosi cha wanajeshi 50,000 wakiwemo wapiganaji wa Korea Kaskazini ili kuwatimua wanajeshi wa Ukraine kutoka eneo la Kursk nchini Urusi.