1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taasisi za kiraia zaukosoa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria

2 Desemba 2016

Zaidi ya makundi 200 ya haki za binaadamu leo hii yametoa mwito kwa baraza kuu la Umoja huo kuuelezea mzozo wa Syria, huku yakilitupia shutuma Baraza la usalama la Umoja kushindwa kukabiliana na mzozo huo.

https://p.dw.com/p/2Tcqc
Syrien Aleppo Trümmer Kinder Ruinen
Picha: Reuters/A. Ismail

Kwenye maazimio yaliyofikiwa na kuwekewa saini na makundi hayo yapatayo 223 na baadae kutolewa jijini New York Marekani, yamelishitumu Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa kusema limewaangusha raia wa Syria, kwa kukosa uwezo wa kushawishi serikali ya Syria kusimamisha uvamizi wake dhidi ya  Aleppo.

Makundi hayo yametaka nchi wanachama 193 za Umoja huo wa Mataifa kuitisha mkutano maalumu wa dharura wa baraza kuu la Umoja huo ili kutoa msukumo wa kumalizwa kwa mashambulizi hayo mjini Aleppo na maeneo mengine nchini Syria, ikiwa ni pamoja na kuruhusu kufikishwa kwa misaada ya kibinaadamu kwenye maeneo yaliyozingirwa.

Makundi hayo yamesema, nchi hizo wanachama pia zinazakiwa kuwakamata wahusika wa mashambulizi hayo yaliyosababisha uhalifu wa kibinaadamu chini ya sheria za kimataifa ili washitakiwe. Hatua hiyo inaunga mkono mkakati uliozinduliwa na Canada, ambao tayari umehamasisha nchi 73 kuto amsukumo wa kuitishwa kikao cha dharura cha baraza la usalama la Umoja wa mataifa kuhusu Syria.

Schweiz Jan Egeland Syrien-Sonderbeauftragter UN
Mjumbe maalumu na mshauri wa masuala ya Syria, Jan Egeland.Picha: UN Photo/J.-M. Ferré

Katika hatua nyingine Umoja Mataifa umesema upo kwenye mazungumzo na Urusi yanayolenga kuandaliwa kwa njia salama ili kufikisha misaada ya kibinaadamu katika eneo la Mashariki mwa Aleppo, pamoja na kuwaondoa raia waliokwamna kwenye eneo hilo lililozingirwa. Umoja huo una kiasi cha tani 150,000 za chakula.

Mashauri wa masuala ya Syria ndani ya Umoja huo, Jan Egeland amesema njia kama jhizo zilifunguliwa katika siku za nyuma, ingawa ni watu wachache waliofanikiwa kupita. Katika kipindi cha hivi karibuni, imekuwa ni vigumu kwa kuwa majeshi ya Syria yanayosaidiwa na Urusi yamesogeza mashambulizi na kushikilia baadhi ya maeneo ambayo awali yalikuwa mikononi mwa waasi. 

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Staffan de Mistura Alhamisi hii alinukuliwa akisema kwamba kiasi ya watu mia tatu walikuwa wakipata misaada baada ya kukimbia eneo hilo la Mashariki mwa Aleppo. Umoja huo uliwahi kutoa mwito wa kusimamishwa kwa mapigano ili kuruhusu misada ya kibinaadamu kuwafikia raia, ombi ambalo lilikataliwa na Urusi na Syria, na badala yake Urusi ilitoa suluhu ya kuwepo kwa njia za kupitisha misaada hiyo.

Mwandishi: Lilian Mtono.
Mhariri: Josephat Charo
  
http://www.dw.com/en/un-russia-proposes-exit-corridors-for-east-aleppo/a-36602570