1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSyria

Syria: Safari za ndege za kimataifa Damascus kuanza tena

4 Januari 2025

Syria imesema kuwa uwanja mkuu wa ndege nchini humo katika mji mkuu Damascus utaanza tena kutumika kwa safari za kimataifa wiki ijayo. Safari za ndani za ndege pia zimerejea.

https://p.dw.com/p/4ooq1
Uwanja wa ndege wa kimataifa mjini Damascus
Safari za kibiashara zilikuwa zimesitishwa kufuatia kuondolewa madarakani kwa rais Bashar al-AssadPicha: Anwar Amro/AFP

Safari za aina hiyo za kibiashara zilikuwa zimesitishwa kufuatia kuondolewa madarakani kwa rais Bashar al-Assad mwezi uliopita. Shirika la habari la umma SANA limesema safari za kuingia na kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa mjini Damascus zitaanza Jumanne wiki ijayo.

Likimnukuu mkuu wa Mamlaka ya Safari za Anga, shirika la SANA limesema serikali imeanza awamu ya kufanya matengenezo kwenye viwanja vya Aleppo na Damascus kwa msaada wa washirika wake ili viweze kuzikaribisha ndege kutoka kote ulimwenguni. Ndege za kimataifa za misaada na wajumbe wa kigeni wa kidiplomasia tayari wamekuwa wakitua nchini Syria. Safari za ndani za ndege pia zimerejea.